MIAKA ELFU
Iwe miaka elfu, kipande cha kusubiri,
Fahamu sinayo hofu, nakuacha ufikiri,
Jibu lako kisharifu, nipa ukiwa tayari.
Fahamu sinayo hofu, nakuacha ufikiri,
Jibu lako kisharifu, nipa ukiwa tayari.
Maili elfu moja, ni mbali nawe tuyuri,
Nimo njiani nakuja, tena sinaye bairi,
Hata yavimbe mapaja, siachi hii safari.
Nimo njiani nakuja, tena sinaye bairi,
Hata yavimbe mapaja, siachi hii safari.
Wawepo ndege alfu, nakupa moja nambari,
Weye tuyuri furufu, kwako sinayo hiyari,
Utaniingia ufu, jibu likiwa si zuri.
Weye tuyuri furufu, kwako sinayo hiyari,
Utaniingia ufu, jibu likiwa si zuri.
Tamati kikwi si hoja, hili naomba kariri,
Moyo wako naungoja, laili wa n'nahari,
Uje ukae pamoja, na wangu kwenye suduri.
Moyo wako naungoja, laili wa n'nahari,
Uje ukae pamoja, na wangu kwenye suduri.
Ushuhuda
ReplyDeleteNilivunjika kabisa uhusiano wangu ulipoisha. Niliamini kweli nimepoteza upendo wa maisha yangu milele. Kisha nikampata Dk. Dawn, na kila kitu kilibadilika.
Kwa fadhili, hekima, na mwongozo wenye nguvu, alinirudishia upendo ambao nilifikiri umetoweka. Leo, tuna furaha zaidi kuliko hapo awali!
Dr. Dawn kweli aligeuza machozi yangu kuwa furaha.
Dk. Dawn Anaweza Kukusaidia Na:
✅ Maneno ya mapenzi
✅ Tahadhari za Ujauzito
✅ Kurejesha Ndoa/Mahusiano
✅ Dawa za mitishamba kwa VVU, Ugonjwa wa Figo, Magonjwa ya Moyo, Maambukizi na mengine mengi.
📧 Barua pepe: dawnacuna314@gmail.com
📞 Simu/WhatsApp: +2349046229159
Usiteseke kimya kimya. Dk. Dawn anaweza kurudisha furaha katika maisha yako!