MPENZI RUDI NYUMBANI
1.
Mie nipo fikirani, mawazo yangu ya mbali,
Sijui mkosi gani, nikaibinua stuli,
Matone ya zafarani, katika kanzu na shali,
Si urongo ni kweli, mwenzako sina amani.
2.
Mekukumbuka fulani, usiku mie silali,
Sijiwezi tabaani, siioni afadhali,
Tonge halendi kinywani, zanipwaya suruali,
Nimekonda kwelikweli, thama ni wewe jamani.
3.
Siko vizuri kitwani, nenda rukwa na akili,
Mwenzako kiza sioni, sipokuwa Ziraili,
Roho yangu ishakani, kupona sina dalili,
Sihitaji sipitali, namtaka wangu hani.
4.
Mambo hayendi kazini, zimesimama shughuli,
Hunitoki akilini, kutwa naona thakili,
Naenda ovyo njiani, nikiwa na idhilali,
Peke una ikibali, kupunga wangu shetani.
5.
Nyonda hebu pulikani, sinitende ukatili,
Hutotoka hatiani, roho ikiwacha mwili,
Nakwambia si utani, hulikwepi zigo hili,
Niikikata kauli, wapata faida gani?
6.
Sita nafunga uneni, fahamu huna badili,
Turudi kama zamani, makosa nayakubali,
Nyongo mkalia ini, fahamu sinayo hali.
Hebu fanya kulla hali, mpenzi rudi nyumbani.

Kazi nzuri ndugu
ReplyDeleteIko poa
DeleteTumsupporti
DeleteKazi nzito sana
ReplyDeleteThanks for sharing information dear.. Hindi Neeti
ReplyDeleteThanks for sharing information dear..it is quite good overweight stocks
ReplyDeleteNice one
ReplyDeletehttps://www.dreamstime.com/extrinsicshopify09_info
ReplyDelete